7 Juni 2026 - 10:54
Source: ABNA
Kufichuliwa kwa maelezo mapya ya wimbi la ujasusi wa Israel dhidi ya maafisa wa Marekani

Gazeti la New York Times limefichua maelezo mapya ya wimbi la ujasusi la utawala wa Israel dhidi ya Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, gazeti la New York Times katika ripoti ya kina lilifichua maelezo ya mgogoro wa kipekee wa kijasusi kati ya Washington na Tel Aviv ambao ulifanya Pentagon kuongeza kiwango cha tishio hadi cha hatari. Huku kukiwa na madai ya kufanywa kwa upenyezaji na operesheni kubwa za udukuzi wa simu za kibinafsi na ofisi za wajumbe na washauri wakuu wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa ripoti hii, uchunguzi wa usalama wa Pentagon umebaini wasiwasi mkubwa kuhusu majaribio makubwa ya Tel Aviv kufanya ufuatiliaji wa kielektroniki na kimwili kwa maafisa wakuu wa Marekani. Watu hao wanajumuisha Steve Witkoff, mjumbe maalum wa Trump; Colby, mshauri mkuu wa sera wa Pentagon; na Michael Demino, naibu wake ambaye ana jukumu la moja kwa moja la kuunda sera za Pentagon katika Mashariki ya Kati.

Katika ripoti hii kwa kurejelea vyanzo vya usalama vya Marekani imesisitizwa kuwa, nia za utawala nyuma ya wimbi hili kali la ujasusi ni kufichua mkakati wa Trump na kuelewa mifumo ya ndani na misimamo inayobadilika ya utawala wake kuhusu mazungumzo na njia ya kisiasa na Iran.

New York Times imeonya kuwa, kuongeza kiwango cha tishio la ujasusi kutasababisha vikwazo vipya vikali vya Pentagon kuzuia kushiriki taarifa na maafisa wa Kizayuni.

Ripoti hii imerejelea maelezo muhimu yaliyohifadhiwa na Wakala wa Ujasusi wa Ulinzi wa Marekani (DIA) kuhusu mbinu za upenyezaji. Imetaja matukio kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa maafisa wa ujasusi wa kijeshi wa utawala walipokuwa wakijaribu kupandikiza vifaa vya kusikilizia ndani ya makao makuu ya wakala mwaka 2021. Pia imeripotiwa kuwa jaribio la maafisa wa Shin Bet wa Israel kupandikiza vifaa vya kusikilizia kwenye gari la Huduma ya Siri (Secret Service) inayohusika na kulinda wakuu wa nchi na wajumbe wa kidiplomasia lilizimwa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha